Mtima wangu wazi

Leo kama jana nahangaika kupata,
Hapa kule kutafuta wa kuwa naye natumai nitampata,
Sitauma makucha ila naomba nipate aliye kama yeye ata kama si mapacha,
Milele niwe naye mapenzi makali moyoni,
Kama hana vioja sitamsumbua ata siku moja,
Kabila yake si shida ila tu awe wa kuvutia,
Nitambamba na tutakuwa kimoja ni kama tumefungwa na kamba,
Njugu karanga ni za kuonja lakini yeye ni mmoja wa kukaanga,
No wonder mimi huitwa mkora labda mimi ni mjanja,
Ilhali sina mkwanja lakini najua nampenda kushinda kina karanja,
Si kujigamba kwa sababu ata kama umati umejaa kwa kiwanja ni yeye ndiye nitapita naye wa kwanza,
Bidii ya mchwa ndio niko nayo kila kukikucha,
Sitamwingisha kwa briefcase instead nitamweka kwa safe,
I will be at peace because my her will be her resting place.

Comments

Popular Posts